Nchi za magharibi za kosoa vikali kuapishwa kwa Maduro
11 Januari 2025Mgombea wa upinzani, Edmundo Gonzalez, alidai kushinda uchaguzi wa rais wa Julai, lakini tume ya uchaguzi ilitangaza ushindi wa Maduro kwa asilimia hamsini na moja za kura.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, amesema Maduro "alishindwa" katika uchaguzi wa mwaka jana na kuita sherehe ya kuapishwa kwake kuwa "uapisho wa rais usio halali."
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy ,amesema hatua ya Maduro kusalia madarakani ni ya ulaghai, huku Uingereza ikitangaza vikwazo zaidi kwa watu wanaohusishwa na utawala wa Maduro.
Rais Vladimir Putin wa Urusi amempongeza Maduro kwa kuapishwa tena kuiongoza Venezuela. Miongoni mwa waliohudhuria shehere hiyo ni Spika wa Bunge la Urusi, Vyacheslav Volodin, Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba na Rais Daniel Ortega wa Nicaragua.