1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi 3 za Afrika zafanyia majaribio chanjo ya Malaria

16 Januari 2020

Nchi tatu za Afrika zimeanza majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa Malaria kwa watoto. Nchi hizo ni Kenya, Malawi na Ghana. Chanjo hiyo mpya kwa jina Mosquirix ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa huo kwa asilimia 40

https://p.dw.com/p/3WHvK
Medizin Forschung l Weltweit erste Malaria-Impfkampagne l Impfstoff
Picha: picture alliance/dpa/K.-J. Hildenbrand

Hata hivyo wataalamu wamesema ni vyema kuifanyia majaribio kama sehemu ya kupiga hatua katika vita dhidi ya Malaria.

Matumaini ya kutumia chanjo hiyo ni kwa ajili ya kuwasaidia watoto wadogo katika kipindi ambapo wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupata malaria maishani mwao.

Ugonjwa huo husababisha vifo vya watu 400,000 kila mwaka, robo tatu ya idadi hiyo ni watoto wa chini ya umri wa miaka 5, barani Afrika.

Mpango wa kutoa chanjo hiyo ulianza mwaka jana, na watoto 360,000 wanatarajiwa kupewa chanjo kila mwaka katika nchi hizo tatu. Chanjo ya kwanza hutolewa mtoto akiwa na umri wa takriban miezi mitano, kisha awamu ya mwisho hutolewa mtoto akikaribia miaka miwili.