MigogoroUlaya
NATO yaitaka China kuchagua, ama magharibi au Urusi
25 Mei 2024Matangazo
Stoltenberg ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild kwamba, China haiwezi kusimama pande zote mbili, wakati ikilenga kuimarisha ushirikiano na magharibi, na kwa upande mwingine ikichochea vita barani Ulaya.
Amesema kuna ongezeko kubwa la mauzo ya vifaa vya mashine na teknolojia nyingine ambazo Moscow inazitumia kutengeneza makombora, vifaru na ndege za kivita ili kuishambulia Ukraine.
Soma pia: Rais Xi wa China akosoa NATO kabla ya ziara yake ya Serbia
Ingawa hakuna rekodi inayoashiria kwamba China inaiuzia Urusi silaha na risasi, lakini mauzo mengine kutoka China kwenda Urusi yameongezeka tangu vita hivyo vilipoanza mnamo Februari mwaka 2022.