Haki za binadamuIran
Narges Mohammadi aishutumu serikali ya Iran kwa "ukidikteta"
10 Desemba 2023Matangazo
Mohammadi ametoa shutuma hizo katika hotuba iliyotolewa na watoto wake mjini Oslo walipokuwa wanapokea tuzo hiyo kwa niaba yake.
Soma zaidi: Mshindi tuzo ya amani ya Nobeli kuanza mgomo wa kula gerezani
Watoto wake mapacha waliyo na miaka 17 Ali na Kiana, wanaoishi uhamishoni Ufaransa tangu mwaka 2015 walisoma hotuba hiyo iliyopenyezwa kutoka korokoroni iliyosisitiza kuwa watu wa Iran watafanikiwa kuondoa vizuizi na dhuluma dhidi yao.
Narges anayepinga uvaaji wa hijabu wa lazima katika Jamhuri hiyo ya kiislamu na hukumu ya kifo inayotolewa huko amekuwa gerezani tangu mwaka 2021 na hakuweza kupokea tuzo yake.