1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi tuzo ya amani ya Nobeli kuanza mgomo wa kula

10 Desemba 2023

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobeli, Narges Mohammadi ataanza tena mgomo wa kutokula akiwa gerezani nchini Iran wakati familia yake ikitarajiwa kupokea tuzo yake siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/4ZzBg
Narges Mohammadi, mwanaharakati wa Iran
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli 2023 Narges Mohammadi Picha: Reihane Taravati/Middle East Images/AFP via Getty Images

Wakizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Norway kwenye sherehe za mkesha wa tuzo ya Nobel, kaka yake na mumewe Mohammadi, ambaye amefanya kampeni dhidi ya uvaaji wa lazima wa hijabu na hukumu ya kifo nchini Iran, atagoma kula "kwa mshikamano" na watu wachache wa kidini wa Baha'i.

Soma zaidi:  Mpelelezi huru wa UN: Iran inawashikilia wanaharakati kinyume cha sheria

Mume wa mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 51, Taghi Rahmani, aliendelea kueleza kwamba mgomo huo ni ishara ya mshikamano na jamii ya  wachache ya kidini ya Baha'i, na kwamba alisema ataanza mgomo wa kula siku atakapopewa tuzo ya Nobel.

Awali Mohammadi aligoma kula kwa siku kadhaa mwanzoni mwa Novemba ili kupata haki ya kuhamishiwa hospitali bila kufunika kichwa chake.

Mwanaharakati huyo amekamatwa mara 13, kuhukumiwa mara tano kwa jumla ya miaka 31 jela na viboko 154, na kufungwa tangu 2021. Mohammadi ametumia zaidi ya miongo miwili iliyopita ndani na nje ya jela na hajawaona watoto wake, ambao sasa wanaishi Ufaransa kwa miaka minane.