1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo kati ya binadamu na wanyamapori Tanzania

18 Januari 2023

Mashirika yanayohusika na mazingira na maliasili yanatoa wito kwa serikali ya Tanzania kufanya juhudi za kukomesha migogoro baina ya binadamu na wanyamapori. Visa hivyo vimesababisha vifo vya watu 1, 069.

https://p.dw.com/p/4MKNd
Bildergalerie Kenia Maasai Olympiade in Kimana
Picha: Reuters/T. Mukoya

Miezi saba iliyopita majira ya saa 11 alfajiri familia ya ya watu wanne iliongozana kuelekea shambani kama ilivyo familia nyingi za wakulima barani Afrika katika kipindi cha msimu wa kilimo. Watu hao wanne wa familia moja wakazi wa  wilaya ya Kiloso mkoani Mororogo Tanzania hata hivyo, hawakufanikiwa kufika shambani, walivamiwa na tembo na mtu mmoja kati yao aliraruriwa vibaya na kufariki dunia. Watu wa karibu na familia ya marehemu wanaeleza.

Soma pia: Idadi ya wanyama pori ulimwenguni kote yapungua kwa 69%

Symbolbild -Safari
Tanzania ina mbuga nyingi za kitaliiPicha: Fotolia/BlueOrange Studio

Tembo huyo alidaiwa kutokea katika eneo la shamba jingine akiwa anavuka mto kuelekea eneo la Kilombero katika mkoa huo wa Morogoro, na tukio hilo likaweka rekodi ya idadi ya vifo vya binadamu viavyotokana na wanayapori kuendelea kuripotiwa hasa katika makazi yanayopakana na mapori au yale yaliyohifadhiwa. 

Inaelezwa kwamba visa vinavyotokana na migogoro baina ya wanayapori na binadamu imesababisha vifo vya watu 1, 069 ambavyo ni sawa na uwiano wa mtu mmoja kuuwawa kila baada ya masaa 52,  pamoja na kuharibu hekta 41,404 za mazo nchini Tanzania kulingana na ripoti ya mwaka 2020, ya mkakati wa kitaifa wa kudhibiti migogoro baina ya wanayamapori na binadamu. Ripoti hiyo  ilinukuu takwimu za wizara ya maliasili na utalii ya Tanzania zilizotolewa kati ya mwaka 2012 na 2019.

Soma pia:Wafanyabiashara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Mbali na juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania za kukomesha vifo  hivyo lakini mashirika ya binafsi yanayohusika na mazingira na maliasili yamekuwa yakifanya juhudi hizo kwa kushirikiana na serikali kama anavyofafanua zaidi hapa John.

Mbali na vifo vya binadamu lakini pia takwimu hizo zinaonesha kuwa wanyamapori 792 waliuwawa katika kipindi hicho.

Veronica Natalis, DW Arusha