Myanmar: UN imerekodi madai yasiokuwa na msingi dhidi yake
10 Aprili 2024Katika taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Global New Light nchini humo, wizara ya mambo ya nje imesema azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo wa Mataifa lililopitishwa wiki iliyopita kukosoa ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu nchini humo lilijumuisha madai yasiokuwa na msingi na kwamba nchi hiyo inalipinga vikali.
Guterres "asikitishwa" na mauwaji Myanmar
Serikali hiyo ya kijeshi imeongeza kuwa haikupokea mawasiliano rasmi kuhusu uteuzi wa hivi karibuni wa mjumbe maalumu mpya wa Umoja huo kwa nchi hiyo Julie Bishop, aliyewahi kuhudumu kama waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Australia.
Hata hivyo, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema kwa kuwa uteuzi huo uliofanywa kupitia azimio la Baraza Kuu, haufuati taratibu za mashauriano kama maazimio ya Baraza la Usalama.