1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Höcke kusimama kizimbani kwa kutumia msemo wa Kinazi

13 Septemba 2023

Mwenyekiti wa chama cha mrengo wa siasa kali Ujerumani AfD jimboni Thuringia Björn Höcke, atapaswa kusimama kizimbani kujibu kesi ya madai ya kutumia kauli zilizopigwa marufuku za Kinazi,katika moja ya hotuba zake.

https://p.dw.com/p/4WIh8
Björn Höcke auf AfD-Bundesparteitag in Magdeburg
Picha: imago images

Mahakama ya mkoa ya Halle imesema imemruhusu mwendesha mashtaka kuendelea na hatua ya kufungua kesi dhidi ya mwanasiasa huyo wa chama hicho kinachochukia wageni.  

Höcke anadaiwa kutumia kauli zilizokatazwa,zilizowahi kutumiwa na tawi la wanajeshi maalum wa chama cha Wanazi.

Scholz atoa mwito kwa Ujerumani kuungana kunusuru taifa

Alitumia kauli hizo katika hotuba yake aliyoitowa katika mji wa Merseburg katika jimbo la Mashariki la Saxony-Anhalt mwishoni mwa mwezi Mei mwaka 2021.

Mwendesha Mashtaka amesema,inadaiwa kwamba mwanasiasa huyo alitambuwa fika,  msemo'' Kila kitu kwa Ujerumani'' umepigwa marufuku nchini Ujerumani na  ni kosa kuutumia. 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW