1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKimataifa

Viongozi wa upinzani Venezuela kuanza kuchunguzwa

6 Agosti 2024

Mwendesha mashitaka mkuu wa Venezuela ametangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgombea wa rais wa upinzani, Edmundo Gonzalez, na kiongozi wake, Maria Corina Machado

https://p.dw.com/p/4j9f8
Venezuela | Caracas | Mwanasheria Mkuu Tarek William Saab
Mwanasheria Mkuu Venezuela Tarek William SaabPicha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Uchunguzi huo unahusiana na wito wao kwa jeshi kutomuunga mkono Rais Nicolas Maduro na kuacha kuwakandamiza waandamanaji. 

Taarifa ya Mwanasheria Mkuu Tarek William Saab iliunganisha uchunguzi huo moja kwa moja na rufaa iliyoandikwa na viongozi hao wawili wa upinzani ambayo iliwasilishwa saa kadhaa kabla kuhusu Maduro na waandamanaji waliojitokeza kuzilinda kura zao katika uchaguzi wa Julai 28. 

Soma pia:Umoja wa UIaya hautambui ushindi wa Maduro

Saab amesema Gonzalez na Machado walimtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais ambaye hakuwa yule aliyetangazwa na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, ambayo ndio taasisi yenye dhamana kufanya hivyo. 

Aidha alisema waliwachochea waziwazi maafisa wa polisi na wa jeshi kukiuka sheria za nchi. Rufaa ya maandishi ya Gonzalez na Machado inaonesha madai ya kufanyika matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyakuzi wa majukumu, usambazaji wa taarifa za uongo ili kusababisha hofu na njama dhidi ya serikali.