Bobi Wine kupasuliwa baada ya kupigwa risasi na polisi
4 Septemba 2024Matangazo
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine atafanyiwa upasuaji, siku moja baada ya kujeruhiwa mguu katika tukio la vurugu ambapo chama chake jana kiliripoti kwamba alipigwa risasi.
Wakili wa mwanasiasa huyo, George Musisi amefahamisha leo Jumatano kwamba hivi sasa hayuko katika hali mbaya ingawa kwa mujibu wa madaktari atafanyiwa upasuaji kuondowa vipande vya bomu la kutowa machozi lililompiga mguuni.
Soma pia: Uganda: Polisi yasitisha mikutano ya siasa ya Bobi Wine
Musisi amesema inaonesha kwenye tukio hilo polisi ililenga kumdhuru mwanasiasa huyo. Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine alipelekwa hospitali ya Nsambya akiwa katika maumivu makali. Jana polisi ya Uganda ilisema itaanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo.