Mwanasiasa mashuhuri Hassan Nassor Moyo afariki dunia
18 Agosti 2020Mzee Moyo atakumbukwa kwa mengi, ikiwemo kuongoza wafanyakazi wa Zanzibar kwenye mapambano ya ukombozi wa visiwa hivyo katika siku za ujana wake.
Soma pia Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa Zanzibar 2010
Moyo alikuwa waziri wa kwanza wa sheria kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia na pia alikuwa muasisi wa muungano na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Zanzibar ambayo baadae yalichangia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Aprili 19, 2015 halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Unguja Magharibi, visiwani Zanzibar, ilkifikia uamuzi w akumvua uanachama wa chama hicho Mzee Moyo, kwa tuhuma za kuchochea kujitenga kwa Zanzibar na mambo mengine.
Soma pia Moyo: Mansoor hakutendewa haki
Licha ya kufukuzwa na chama hicho tawala, Mzee Moyo hakuhamia chama chengine, lakini alikuwa akisisitiza kwamba anamuunga mkono yeyote anayepigania mamlaka zaidi kwa visiwa hivyo ndani ya Muungano wa Tanzania.