Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa Zanzibar 2010
23 Oktoba 2014Kufuatia taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Tanzania juu ya nafasi ya Mzee Moyo kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2010, Josephat Charo alizungumza na mwanasiasa huyo ambaye alikuwa mjumbe kwenye Baraza la kwanza la Mapinduzi la Zanzibar chini ya Marehemu Abeid Karume, Waziri wa Sheria wa Muungano, Waziri wa Elimu wa Zanzibar na sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, juu ya mchango wake huo, hasa kwa kuwa vyombo vya habari viliandika chama tawala cha CCM kilikuwa tayari kwa lolote lakini sio kutangazwa mgombea wa kilichokuwa chama cha upinzani, CUF, kama mshindi wa urais kwenye uchaguzi huo.
Katika mahojiano haya, Mzee Moyo kwanza anaelezea vipi aliweza kumshawishi mgombea wa CUF, Seif Sharif Hamad, akubali ushindi wa mpinzani wake mgombea wa CCM na rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman