JangaAfghanistan
Mvua yasababisha vifo vya watu 15 Afghanistan
26 Mei 2024Matangazo
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Afghanistan imesababisha vifo vya watu 15 wakiwemo watu 10 wa familia moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Familia hiyo, inayojumuisha wazazi na watoto wao wanane, wanaripotiwa kupoteza maisha eneo la Faizabad, mji mkuu wa mkoa wa Badakhshan.
Soma pia: Watu 84 zaidi wapoteza maisha Afghanistan kwa mafuriko
Mkurugenzi wa idara ya kukabiliana na majanga katika mkoa huo Mohammad Akram amesema timu ya uokoaji imefanikiwa kuupata mwili wa mama pekee.
Mafuriko na mvua zimesababisha uharibifu mkubwa ikiwemo maafa ya mamia ya watu katika sehemu nyingi ya nchi hiyo ya bara Asia.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuwa manusura wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.