Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu wengine 29 Afghanistan
20 Aprili 2024Msemaji wa idara hiyo, Janan Sayeq, amesema watu hao 29, walifariki dunia kwenye mikoa 10 tofauti kutokana na mvua hiyo kubwa iliyoanza kunyesha siku ya Jumatano hadi leo Jumamosi.
Soma pia:Maporomoko ya udongo yaua zaidi ya watu 30 Afghanistan
Sayeq ameongeza kuwa watu wengine saba walijeruhiwa katika kipindi hicho na nyumba 72 kuharibiwa huku zaidi ya ekari 2,500 za mashamba zikisombwa.
Watu 25,000 wanahitaji msaada nchini Afghanistan
Kulingana na takwimu rasmi, zaidi ya watu 100 wamefariki katika mafuriko mwezi huu huku zaidi ya familia 25,000 zikihitaji msaada.
Mwaka uliopita, Umoja wa Mataifa ulionya kuwa Afghanistan inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.
Soma pia:Mamia wafa kwa mafuriko Pakistan, Afghanistan
Baada ya miongo minne ya vita, nchi hiyo iko katika orodha ya mataifa ambayo hayajajiandaa vizuri kukabiliana na hali mbaya ya hewa, ambayo wanasayansi wanasema inazidi kujitokeza mara kwa mara na kuwa mbaya zaidi.