Museveni akemea shinikizo la Benki ya Dunia kusitisha mikopo
10 Agosti 2023Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameishutumu Benki ya Dunia kwa kutumia pesa kujaribu "kuishinikiza" serikali juu ya sheria yake yenye utata dhidi ya mashoga na kusisitiza kuwa hawahitaji shinikizo kutoka kwa mtu yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo katika jamii yao.
Museveni aliyetia saini sheria hiyo dhidi ya mashoga, amesema Waganda watajiendeleza kwa kupewa mikopo au la, akisema inasikitisha kuona Benki ya Dunia wanathubutu kuwalazimisha kuacha imani, utamaduni, kanuni na uhuru wao kwa kutumia pesa.
Benki ya Dunia ilisema siku ya Jumanne kuwa Sheria ya Uganda ya Kupinga Ushoga "kimsingi inakinzana" na maadili ya taasisi hiyo na kwamba inasitisha mikopo kwa taifa hilo na hakuna ufadhili mpya wa umma utakaowasilishwa kwa bodi yake ya wakurugenzi ili kuidhinishwa kwa sasa.
Hata hivyo viongozi wa Uganda wamesema wanaendelea mazungumzo na Benki ya Dunia.