Operesheni ya kukabiliana na uhalifu kwenye eneo tete la Baringo magharibi ya Kenya imeanza kwa amri ya serikali ya kuwapiga risasi na kuwauwa wahalifu wote wanaotumia bunduki. Msimamo huo wa serikali uliotangazwa na kamishnaa wa eneo la Bonde la ufa George Natembeya umeibua wasiwasi iwapo ni njia muafaka ya kuzima uhalifu. Alizungumza na Rashid Chilumba.