1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoItaly

Mshambuliaji wa zamani wa Italia Vialli afariki

6 Januari 2023

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Juventus, Chelsea na Italia Gianluca Vialli amefariki akiwa na umri wa miaka 58. Klabu yake ya zamani ya Sampdoria imetangaza kwamba Vialli ameaga dunia kutokana na saratani ya kongosho.

https://p.dw.com/p/4LoUq
Gianluca Vialli, italienischer Nationalspieler verstorben
Picha: Marco Canoniero/imago images

Mshambuliaji huyo wa zamani alisemekana kwamba anaugua saratani mwaka 2017 ila alikuwa na dhima kubwa katika kampeni ya Italia ya kushinda Kombe la Ulaya mwaka 2021 ambapo alimsaidia aliyekuwa mshambuliaji mwenzake wa muda mrefu katika klabu ya Sampdoria na kocha wa timu hiyo ya taifa Roberto Mancini. 

EURO 2020 | Italien vs Österreich | Tor Chiesa
Vialli akikumbatiana na Roberto ManciniPicha: Laurence Griffiths/REUTERS

"Pamoja tumetoka mbali, tumekuwa na kutafuta, tumeshinda na kuwa na ndoto pamoja. Ulikuja kama mvulana ila sasa tunakupigia saluti kama mwanamume," ilisema taarifa ya klabu ya Sampdoria.

Alipata umaarufu katika klabu hiyo ya Sampdoria ambayo aliichezea kwa misimu minane ambapo alishinda taji la Serie A na Kombe la Vila Bingwa Ulaya kabla kujiunga na Juventus mwaka 1992 kwa kitita cha yuro milioni 16.5 ambacho ilikuwa ni rekodi wakati huo.

Alishinda Kombe la Vila Bingwa Ulaya akiwa na Juventus kabla kujiunga na Chelsea 1996 ambapo mwaka 1998 aliishia kuwa mchezaji na kocha wakati huo huo baada ya Ruud Gullit kuachishwa kazi.

Gianluca Vialli, italienischer Nationalspieler verstorben
Vialli alipokuwa mchezaji wa ChelseaPicha: imago images/Sportfoto Rudel

Aliiongoza Chelsea kushinda kombe la FA mwaka 2000 ila msimu uliofuata akaachishwa kazi.

Chanzo/AFP