Ujerumani: Kauli za Musk haziwezi kuisumbua Ujerumani
6 Januari 2025Matangazo
Ujumbe huo wa msemaji wa serikali umetolewa siku chache baada ya Musk kumkosoa Kansela wa Ujerumani Olaf Schoz na kusema kwamba anakiunga mkono chama cha mrengo wa kulia kinachojiita mbadala kwa Ujerumani cha AFD kwenye uchaguzi ujao wa Ujerumani. Akigusia matamshi hayo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema."Jambo muhimu ni kwamba Bwana Musk ameunga mkono upande wa chama chenye siasa kali za mrengo wa kulia na, kama unavyoona, hayafanyi hayo katika nchi hii tu. Jambo hilo hatukubaliani nalo, na pia nalipinga." Viongozi wengine katika mataifa ya Ulaya ikiwemo Uingereza, Norway na Ufaransa wameonyesha kukerwa na kukemea kauli za bilionea huyo katika mtandao wake wa X.