1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Kiongozi wa upinzani nchini India Rahul Gandhi apiga kura

25 Mei 2024

Kiongozi wa upinzani nchini India Rahul Gandhi amepiga kura hii leo wakati uchaguzi unaofanyika kwa wiki sita nchini humo ukirejea tena.

https://p.dw.com/p/4gHRO
India, New-Delhi | Rahul na Sonia Gandhi wakitoka kupiga kura
Rahul Gandhi mgombea wa upinzani nchini India akiwa na mama yake Sonia Gandhi wakitoka kwenye kituo cha kupigia kura mjini New Delhi, Mei 25, 2024Picha: Arun Sankar/AFP

Mpinzani huyo wa Waziri Mkuu Narendra Modi ameishutumu serikali kwa kuwalenga isivyo halali na kuwashitaki kwa makosa ya uhalifu.  

Gandhi, ambaye ni kiongozi maarufu zaidi wa chama cha upinzani cha Congress amepiga kura yake katika kituo kilichopo New Delhi.

Gandhi ambaye pia ni mjukuu wa Waziri Mkuu wa zamani amesema baada ya kupiga kura kwamba Modi ameanzisha mkakati hatari na kuongeza kuwa analenga kuwapeleka jela viongozi wote wa upinzani.

Matarajio ya Modi, yameimarishwa zaidi na uchunguzi wa uhalifu aliouanzisha dhidi ya wapinzani wake, hatua inayoibua wasiwasi kwa Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk pamoja na makundi ya haki za binaadamu ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.