1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani wa rais Maduro akabiliwa na uchunguzi wa kisheria

27 Agosti 2024

Mgombea wa upinzani aliyeshiriki katika uchaguzi wa rais nchini Venezuela, Edmundo Gonzalez Urrutia ameitwa kwa mara ya pili leo katika ofisi ya waendesha mashtaka.

https://p.dw.com/p/4jyby
Mgombea wa upinzani aliyeshiriki katika uchaguzi wa rais nchini Venezuela, Edmundo Gonzalez Urrutia
Mgombea wa upinzani aliyeshiriki katika uchaguzi wa rais nchini Venezuela, Edmundo Gonzalez UrrutiaPicha: Ronald Pena/AFP

Mgombea wa upinzani aliyeshiriki katika uchaguzi wa rais nchini Venezuela, Edmundo Gonzalez Urrutia ameitwa kwa mara ya pili leo katika ofisi ya waendesha mashtaka ,kama  sehemu ya uchunguzi kuhusu madai aliyotowa,kwamba alikuwa mshindi halali wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

soma: Maelfu waandamana Venezuela kupinga ushindi wa Rais Maduro

Gonzalez mwenye umri wa miaka 74 ambaye yuko mafichoni tangu baada ya uchaguzi huo,alipuuza mwito wa mwanzo wa kumtaka afike kwenye ofisi hiyo jana Jumatatu. Kwa mujibu wa mwito uliotolewa,Gonzale Uruttia anachunguzwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kughushi nyaraka za serikali na kutaka madaraka kwa nguvu.

Tume ya uchaguzi ya Venezuela ilimtangaza Nicolas Maduro mshindi wa uchaguzi huo wa rais kwa kupata asilimia 52, lakini ilikataa kuchapisha matokeo,ikidai wadukuzi wamehujumu data za matokeo.Upinzani ulichapisha matokeo ya vituo vyote na kuonesha mgombea wao Edmundo Gonzalez alishinda kwa asilimia 67 ya kura.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW