1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gonzalez atiwa hatiani Venezuela

8 Agosti 2024

Mahakama ya Juu ya Venezuela imemtia hatiani aliyekuwa mgombea urais, Edmundo Gonzalez, kwa kukiuka amri halali ya mahakama hiyo.

https://p.dw.com/p/4jDow
Edmundo Gonzalez, aliyekuwa mgombea urais wa upinzani nchini Venezuela.
Edmundo Gonzalez, aliyekuwa mgombea urais wa upinzani nchini Venezuela.Picha: Pedro R. Mattey/Anadolu/picture alliance

Gonzalez, anayedai kumshinda Rais Nicolas Maduro kwenye uchaguzi wa hivi karibuni, alikataa kuhudhuria mahakamani hapo kwenye kikao cha kuthibitisha matokeo ya uchaguzi huo hapo jana.

Kwa hukumu hiyo, sasa mwanadiplomasia huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 74, anakabiliwa sasa na kifungo cha hadi siku 30 jela, kwa mujibu wa mawakili wake.

Soma zaidi: Umoja wa UIaya hautambui ushindi wa Maduro

Akiandika hapo jana kwenye mtandao wa X, Gonzalez alisema kuhudhuria mahakamani kungelimuweka kwenye hatari na kuuweka rehani uamuzi wa wapiga kura wa Venezuela waliouchukuwa tarehe 28 Julai.

Tume ya uchaguzi wa Venezuela, ambayo inakosolewa na upinzani kwa kumpendelea Maduro, ilimtangaza kiongozi huyo kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 51, bila ya kuchapisha matokeo halisi ya kura.