1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja auwawa katika shambulizi kanisani Istanbul

28 Januari 2024

Watu wawili wamelishambulia kwa risasi kanisa Kikatoliki la Santa Maria la mjini Istanbul, Uturuki wakati wa misa.

https://p.dw.com/p/4bleU
Uturuki Istanbul | Kanisa la Santa Maria
Polisi wakipiga doria nje kanisa la Santa Maria baada ya shambuliziPicha: DHA

Akitoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii, Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema mtu mmoja aliyekuwa akihudhuria ibada hiyo na aliyetambuliwa kwa jina C.T aliuwawa katika tukio hilo.

Watu wengine kadhaa wameripotiwa kuwa wamejeruhiwa.

Yerlikaya ameeleza kuwa shambulio hilo lilifanywa na watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao ambao walifanikiwa kukimbia baada kufyatua risasi na kwamba uchunguzi wa kuwabaini wahusika umeanza.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametuma salamu za rambi rambi baada ya shambulio hilo na kusema kuwa hatua zinazohitajika zimechukuliwa ili kuwapata wauwaji haraka iwezekanavyo.

Naye Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, amelizungumzia tukio hilo katika misa ya Jumapili na kusema yuko pamoja na jumuiya ya kanisa lililokumbwa na mkasa huo.