1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais Korea Kusini ajiuzulu

10 Januari 2025

Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Rais wa Korea Kusini, Park Chong-jun, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Kaimu Rais, Choi Sang-mok.

https://p.dw.com/p/4p1A3
Korea Kusin | Park Chong-jun
Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais Park Chong-jun.Picha: Yonhap via REUTERS

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Kaimu Rais imeeleza kuwa Park kwa sasa anachunguzwa kwa kuzuia juhudi za wiki iliyopita, za maafisa wa kupambana na rushwa kumkamata Rais Yoon Suk Yeol ambaye aliondolewa madarakani na bunge. 

Choi, ameikubali barua ya Park kujiuzulu katika nafasi hiyo.

Soma pia: Maafisa Korea Kusini wajaribu kumkamata Rais Yoon

Wakati huo huo, Kaimu Rais wa Korea Kusini ametoa wito wa kuwepo makubaliano kati ya vyama tawala na upinzani kuhusu muswada maalum wa mwendesha mashtaka kwa lengo la kuutatua mzozo unaoendelea wa kukamatwa kwa Yoon.