Mkutano wa kimataifa wa amani Ukraine wafungua Uswisi
15 Juni 2024Viongozi wa kitaifa na wawakilishi wengine wa ngazi za juu kutoka mataifa 92 na mashirika ya kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kujadili masuala kuanzia usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine, usalama wa mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhya unaokaliwa na vikosi vya Urusi na masuala ya kitu, ikiwemo kubadilishana wafungwa.
Urusi hata hivyo haijaalikwa kwenye mkutano huo. Marekani ambayo ndiyo mshirika muhimu zaidi wa Ukraine, inawakilishw ana makamu wa Rais Kamala Harris. Viongozi kadhaa wa Ulaya wanahudhuria pia, wakiwemo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Urusi kwa sasa inakalia karibu humusi moja ya ardhi ya Ukraine, ikiwemo Rasi ya Crimea iliyoinyakua mwaka 2014. Rais Vladmir Putin aliitaka Ukraine kukabidhi maeneo ya Donetsk, Luhansk, Kherson, Zaporizhzhya na rasi ya Crimea kama sharti la kukomesha vita, masharti ambayo Kyiv imeyataja kuwa ya kipuuzi.