Mkutano wa amani kuhusu Ukraine kufunguliwa leo Uswisi
15 Juni 2024Mkutano huo utakaohudhuriwa na Wakuu na wawakilishi wa ngazi za juu wa serikali kutoka mataifa takriban 100, pamoja na mashirika ya kimataifa unatarajiwa kujadili masuala kadhaa, ikiwemo usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine, usalama wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya kinachodhibitiwa na Urusi kwa sasa pamoja na masuala mengine ya kiutu ikiwemo kubadilishana wafungwa.
Mkutano huo ambao unafanyika kwa jitihada za Ukraine utahudhuriwa na Rais Volodymyr Zelensky akiambatana na viongozi wengine ambao wanatokea kwenye mkutano wa viongozi wa G7 nchini Italia ambao nao ulijikita kujadili vita vya Urusi nchini Ukraine.
Soma pia:Biden, Zelensky wasaini mkataba wa ´kihistoria´ wa usalama
Pia mkutano huo wa siku mbili unalenga kuihamasisha jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa serikali mjini Kyiv ikiwa ni pamoja na kutoka nchi ambazo ni rafiki kwa Urusi.