Viongozi wa G7 kujadili uhamiaji, Afrika na akili mnemba
14 Juni 2024Mada zitakazojadiliwa hii leo ni pamoja na uhamiaji, kanda ya Indo-Pasifiki na usalama wa kiuchumi Afrika na teknolojia ya akili ya kubuni miongoni mwa nyingine.
Viongozi hao pia wanatarajiwa kuelezea wasiwasi kuhusu uwezo wa kiviwanda wa China uliopitiliza na uungwaji wake mkono kwa Urusi.
Biden, Zelensky wasaini mkataba wa ´kihistoria´ wa usalama
Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis atahudhuria kikao cha leo ambapo atatoa hotuba kuhusu hatari na uwezo wa teknolojia ya akili ya kubuni.
Viongozi kadhaa kutoka mataifa yasio wanachama wa G7 watahudhuria mkutano huo, wakiwemo waziri mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Kenyan William Ruto, miongoni mwa wengine.