Njia za kumaliza vita vya Urusi na Ukraine zajadiliwa Uswisi
16 Juni 2024Mkutano huo pia utaangalia athari ya vita kwa maisha ya binaadamu.
Rasimu iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, inauelezea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kama vita, jambo ambalo Moscow inaendelea kulikanusha ikisema ni operesheni maalum ya kijeshi. Rasimu hiyo pia imetoa wito wa kuachiwa kwa kinu cha nyuklia cha Ukraine kinachodhibitiwa na Urusi cha Zaporizhzhia pamoja na bandari ya Azov.
Vita vya Urusi nchini Ukraine vimeendelea kusambaratisha uhusiano wa taifa hilo na nchi za Magharibi ambapo Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema mataifa hayo yanataka kuifanya Urusi kuyanyenyekea.
Mkutano wa kimataifa wa amani Ukraine wafungua Uswisi
Viongozi wa dunia akiwemo makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekusanyika katika eneo la la mapumziko la Bürgenstock ili kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa wa kumaliza vita hivyo.