SiasaAsia
Mkutano muhimu wa chama tawala cha China waanza Beijing
15 Julai 2024Matangazo
Mkutano huo unafanyika mjini Beijing katika wakati ambapo China imeshuhudia ukuaji mdogo wa kiuchumi kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya pili ya mwaka wa kiuchumi.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili namna ya kukabiliana na kuporomoka kwa ukuaji wa uchumi, kutokana na kushuhudiwa mgogoro wa madeni katika sekta ya biashara ya ujenzi wa majumba, kupungua ununuaji wa mahitaji na kuongezeka kwa idadi ya wazee.
Mivutano ya kibiashara na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya pia imechangia kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa China ambapo takwimu rasmi zinaonesha kwamba nchi hiyo ininayoshika nafasi ya pili kiuchumi duniani uchumi wake ulistawi kwa asilimia 4.7 pekee katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka.