1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China ina lengo la kukuza uchumi kwa asilimia 5, 2024

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

China imetangaza hii leo kuwa inalenga kufikia ukuaji uchumi wa karibu asilimia tano kwa mwaka huu wa 2024, lengo ambalo viongozi wa taifa hilo la pili kwa uchumi duniani wamekiri kuwa litakuwa ni changamoto kulifikia.

https://p.dw.com/p/4dApH
Uswisi | Kongamano la Kiuchumi la Dunia 2024 huko Davos
Li Qiang, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, akihudhuria hafla ya ufunguzi. Mkutano wa kila mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani unachukuliwa kuwa moja ya sehemu muhimu zaidi za mikutano ya wanasiasa wakuu.Picha: Hannes P Albert/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametangaza mipango hiyo na sera muhimu za serikali kwa mwaka 2024, wakati bunge la China likifungua kikao chake cha kila mwaka. Akihutubia maelfu ya wajumbe, Li ameonya kwamba kutakuwa na changamoto kufikia malengo hayo. "Kufikia malengo ya mwaka huu haitakuwa rahisi, kwa hivyo tunahitaji kudumisha umakini wa sera, kufanya kazi kwa bidii zaidi, na kuhamasisha juhudi za pamoja za pande zote." China imeapa kusimama kidete dhidi ya Taiwan na kupinga juhudi zozote za kujipatia uhuru.