1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri na Marekani zajadili usitishaji mapigano Gaza

9 Julai 2024

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi na mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA William Burns wamejadili kuhusu juhudi za kufikia usitishaji mapigano Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4i4aV
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi Picha: Jacquelyn Martin/Pool/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya rais wa Misri imefahamisha kwamba Al Sisi amethibitisha msimamo wa nchi yake wa kupinga operesheni ya kijeshi kuendelea Ukanda wa Gaza.

Mashambulizi makali ya Israel yameutikisa mji wa Gaza City leo Jumanne huku maelfu ya Wapalestina wakiendelea kutafuta hifadhi. 

Leo kundi la wanamgambo la Hamas limesema ikiwa Israel itaendelea na mashambulizi yake yaliyoanza Jumatatu dhidi ya Gaza, mazungumzo ya kusitisha vita na kuachiliwa kwa wafungwa huenda yakasambaratika. 

Soma pia:UN yapinga wapalestina kuhamishwa Gaza

Hata hivyo taarifa zinasema mazungumzo hayo ya mjini Doha yataanza tena kesho Jumatano na baadae kuhamishiwa  mjini Cairo Alhamisi kufuatia mazungumzo yaliyofanyika leo kati ya rais Sisi na mkurugenzi wa CIA William Burns.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW