MigogoroLibya
Miili 11 ya wanaodhaniwa wahamiaji yaokolewa pwani ya Libya
8 Juni 2024Matangazo
Kundi hilo limeandika kupitia mtandao wa X kwamba miili hiyo ilipatikana baada ya msako wa masaa tisa uliofanywa na timu ya uokozi ya GeoBarents.
Madaktari hao waliarifiwa juu ya miili hiyo na shirika lisilo la serikali la Ujerumani la Sea-Watch ambalo mapema jana Ijumaa lilisema liliona miili 11 ya watu ikielea majini.
Kulingana na Sea-Watch, serikali ya Libya kupitia kikosi cha uokozi kinachofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, iliamua kuiacha miili hiyo baharini.
Makundi hayo kwa pamoja yamezilaumu nchi za Ulaya kwa vifo hivyo, kutokana na sera zake ngumu za uhamiaji.