Mgonjwa anayeshukiwa kuwa na mpox agunduliwa Brazil
27 Agosti 2024Kituo hicho kimesema kupitia taarifa kuwa, abiria aliyekuwepo katika eneo maalum kwenye uwanja huo wa ndege lililotengwa kwa ajili ya watu wanaosubiri kuomba hadhi ya ukimbizi tangu mapema mwezi huu, ameonyesha dalili zinazofanana na ugonjwa wa homa ya nyani.
Anvisa hata hivyo haikutoa maelezo juu ya sehemu alikotoka au nchi ya asili ya abiria huyo ambaye baadaye alipelekwa hospitali.
Soma pia: Papa Francis atoa mwito wa msaada zaidi kwa wagonjwa wa mpox
Wizara ya afya nchini Brazil imesema zaidi ya wagonjwa 700 waliothibitishwa kuugua homa ya nyani wameripotiwa kote nchini humo mwaka huu, ingawa hakuna hata mmoja aliyekutwa na aina mpya ya kirusi cha homa ya nyani.
Wiki iliyopita, serikali ya Brazil ilitangaza kwamba itaimarisha sheria za watu kuingia nchini humo ili kuzuia wimbi la wahamiaji wanayoitumia nchi hiyo kama ngazi ya kuingia Marekani na Canada.