Olaf Scholz: Upendeleo wa uhalisi juu ya nafsi
25 Agosti 2021Ilikuja kama mshangao mkubwa baada ya SPD kumteua Olaf Scholzkuwa mgombea wake wa nafasi ya kansela zaidi ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu. Ilikuwa inashangaza hata zaidi kwamba chama hicho kingemchagua Scholz, ambaye miezi michache kabla alikuwa ameshindwa katika mbio za kuwania uongozi wa chama.
Lakini Olaf Scholz anadhihirisha imani isiyotikisika na amehimili misukosuko mingi katika kazi yake ya muda mrefu ya siasa.
Hili lilimuweka katika nafasi nzuri ya kung'aa katika mzozo wa janga la virusi vya corona: Kama waziri wa fedha, anahusika na utoaji wa mabilioni ya euro katika ufadhili wa dharura kusaidia kujenga uchumi na raia kuweza kuhimili dhoruba ya janga hilo.
"Hii ndiyo manati inayohitajika kufanikisha kazi," aliahidi Scholz, kwa mchanganyiko wa ufanisi baridi na imani ya kujimwambafai. "Tunaweka silaha zetu mezani kuonesha kwamba tuko imara vya kutosha kuzishinda changamoto za kiuchumi ambazo tatizo hili linaweza kuzisababisha."
Soma pia: Scholz: Nitahimiza mkakati mpya kuelekea Ulaya Mashariki
Katika nyakati za mzozo, nadharia ya vitendo hujenga haiba kubwa na hilo limemsaidia sana Scholz mwenye umri wa miaka 62.
Haiba ya roboti
Ni tofauti na mwaka 2003 wakati gazeti la kila wiki la Die Zeit lilipompachika jina la utani Scholz la "Scholzomat", mchanganyiko wa jina lake na "Automat", neno la Kijerumani linalomanisha "mashine", likizungumzia tabia ya katibu mkuu huyo wa wakati huo wa chama cha SPD, kutumia misamiati ya kitaaluma.
Kazi ya mashine hii ni kuendelea kuuza sera za SPD. Ilianzia kwenye mpango tata wa mageuzi ya soko la ajira unaojulikana kama 2010, ambao ulikuja na makato makali kwa baadhi ya wapokeaji wa fedha za ustawi wa jamii. Scholz alijikuta akiutetea mpango huo ndani na nje ya chama chake.
"Mimi ndiyo nilipewa kazi ya kueneza ujumbe. Nililaazimika kuonesha kiwango fulani cha kutobadili msimamo," Scholz alisema baadae, na kuongeza kuwa kweli "alijiskia kama afisa. Hakukuwa na namna ya kujitoa."
Soma pia: SPD yamchagua Olaf Scholz kugombea ukansela
Alisema wasiwasi wake wa kwanza haukuwa hisia zake mwenyewe bali haja ya kuonesha "utiifu wa hali ya juu" kwa kansela wa wakati huo na kiongozi wa SPD, Gerhard Schröder, na chama cha SPD chenyewe. "Nilikuwa sijaribu kujiokoa bali kuokoa chama changu."
Kazi isiyo na shukrani
Mwishowe, juhudi za uokozi zilishindwa. Siyo tu SPD ilipoteza ukansela kwa CDU, lakini Olaf Scholz alipata taswira ambayo ilimchukulia muda kujivua: ya mrasimu mwenye kuchosha na kuuwa furaha.
Ndnai ya SPD, watu wengi walipata ugumu kuanza kumpenda bwana huyo kutoka Hamburg ambaye hangeweza kusema zaidi ya kile ambacho kilikuwa kinahitajika hasa.
Ndani ya SPD, watu wengi walikuwa na ugumu wa kupasha moto moto kwa huyu pragmatist wa kweli wa Hamburg ambaye hangesema zaidi ya kile kilichokuwa kinahitajika.
Lakini Scholz alibakia na msimamo wake, na kupanda kimya kimya ngazi ya kisiasa. Alikuwa katibu mkuu wa SPD, waziri wa mambo ya ndani wa jimbo na meya wa Hamburg, na sasa ndiye waziri wa fedhga wa Ujerumani na naibu kansela.
Soma pia: Mkutano mkuu wa SPD wafunguliwa Berlin
Olaf Scholz anachukuliwa kuwa mwanachama wa tawi la kihafidhina la chama -- lakini pia ni mgumu kuhusishwa na matabaka ya kisiasa kama mrengo wa kushoto au mrengo wa kulia. Kama naibu kiongozi wa tawi la vijana la SPD la Jusos, mitizamano yake mingi ilikuwa mikali kijamii na inayokosoa vikali ubepari.
Kujifunza kipengele cha biashara ya burudani
Lakini muda mrefu umepita tangu Scholz ajiunge na SPD kama mwanafunzi wa shule ya upili mnamo 1975 na kuchaguliwa kwake kwenye Bundestag mwaka 1998. Katika miaka hiyo, Scholz aliendesha kampuni yake mwenyewe ya uwakili mjini Hamburg, akibobea katika sheria ya biashara, ambapo alijifunza mengi kuhusu namna uchumi na ujasiriamali vinavyofanya kazi. Hilo liliacha alama yake.
Ilichukua muda mrefu kwa Olaf Scholz kutambua kwamba siasa pia inahusu kuufanya ujumbe wako usikike na kuuza sera zako. Lakini wakati wagombea wa uongozi wa SPD walipozuru nchi wakifanya mdahalo baina yao mwishoni mwa mwaka 2019, waziri huyo wa fedha alionekana kubadilika.
Mwenendo wake ulikuwa wa mhemko zaidi, wa kufunguka zaidi, na juu ya yote wa kirafiki zaidi. Wakati huo huo, hakuficha shauku yake ya kuitaka kazi hiyo. Lakini alipata mshtuko wa kushindwa vibaya na wagombea wawili wa mrengo wa kushoto ndani ya chama - Saskia Esken na Norbert Walter-Borjans.
Pamoja na hayo, askari wa zamani wa chama Scholz alisimama imara. Alibakisha nadhari kwenye kazi yake serikali na kuwaacha viongozi wapya wa SPD kuendeleza chama. Aliendelea kuwa mtiifu kwa chama na kamwe hakugeukia chokochoko -- akiwa salama kwa dhana kwamba uongozi mpya ambao haukuwa na uzoefu wa kiwango chake, ungefanya makosa yao wenyewe.
Katika miezi iliyofuatia uteuzi wake kama kama mgombea mkuu, Scholz ameepuka kufanya makosa makubwa, na kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 15, chama chake cha SPD kimeupiku muungano wa vyama vya kihafhidhina vya CDU/CSU katika uchunguzi wa maoni ya wapigakura.
Chanzo: DW