1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III atarajiwa kulihutubia Bunge la Ufaransa

21 Septemba 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza aliye ziarani Ufaransa anatarajiwa kulihutubia Bunge na kukutana na vikundi vya michezo katika vitongoji vya kaskazini mwa mji wa Paris.

https://p.dw.com/p/4Wd2D
Frankreich König Charles zu Besuch in Paris
Picha: Christian Hartmann/REUTERS

Mfalme huyo pia atalizuru Kanisa kuu la Notre-Dame lililoharibiwa kwa moto. Hapo jana, Mfalme Charles na mkewe Camilla walipokelewa katika siku ya kwanza ya ziara yao kwa sherehe katika "Arc de Triomphe" na kukaribishwa chakula cha jioni na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Versailles.

Mfalme Charles III azitaka Uingereza na Ufaransa kuyapiga jeki mahusiano

Mfalme huyo wa Uingereza ametoa rai kwa mataifa hayo washirika  kuyapiga jeki zaidi mahusiano yao ili kukabiliana na changamoto za karne ya 21, akisema mahusiano ya Ufaransa na Uingereza yameshuhudia kipindi cha msukusuko lakini ni wajibu wa nchi hizo mbili kuyaimarisha tena . 

Rais Macron amemhakikishia Mfalme Charles kuwa licha ya Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, bado itaendelea kuwa sehemu ya kanda hiyo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za pamoja. Ziara ya Mfalme Charles nchini Ufaransa itamalizika kesho Ijumaa.