Uingereza na Ufaransa zaombwa kuimarisha mahusiano yao
21 Septemba 2023Akizungumza wakati ya hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na mwenyeji wake rais Emmanuel Macron, Mfalme Charles amesema mahusiano ya Ufaransa na Uingereza yameshuhudia kipindi cha msukusuko lakini ni wajibu wa nchi hizo mbili kuyaimarisha tena .
Ingawa Mfalme Charles hakulitaja moja kwa moja suala la Brexit ambalo limekuwa chanzo cha mgawanyiko kati ya Uingereza na mataifa washirika wa Ulaya, alisema lakini Uingereza na Ufaransa zimekuwa na historia ndefu iliyojaa vizingiti.
Kwa upande wake rais Macron amemhakikishia mFalme Charles kuwa licha ya Uingereza kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya bado itaendelea kuwa sehemu ya kanda hiyo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za pamoja.
Ziara ya Mfalme Charles nchini Ufaransa ilianza hapo jana mchana na itamalizika kesho Ijumaa.