1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles ahutubia bunge baada ya kupokea rambirambi

12 Septemba 2022

Mfalme Charles III ametoa hotuba yake ya kwanza bungeni tangu kutangazwa rasmi kuwa mfalme akisema bunge ni chombo hai cha demokrasia ya Uingezera.

https://p.dw.com/p/4Gif0
Presentation Of Addresses By Both Houses of Parliament To His Majesty King Charles III
Picha: Henry Nicholls/WPA/Getty Images

Mfalme Charles III wa Uingereza anatarajiwa kujiunga na ndugu zake wa kifalme wakati jeneza ambalo limebeba mwili wa mama yake Malkia Elizabeth II, litakapokuwa likisafirishwa kutoka mojawapo ya makasri yake yaliyoko Scotland hadi kanisa la kihistoria la Giles mjini humo. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa maelfu ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho wakati wa msafara wa kuusafirisha mwili wa hayati Elizabeth II. 

Kabla ya kuelekea Scotland, Mfalme Charles III mwenye umri wa miaka 73, aliyetangazwa mfalme wa Uingerezamoja kwa moja wiki iliyopita kufuatia kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II, ataelekea bunge la taifa la Uingereza kwa hafla nyingine ya kitamaduni, ambapo wabunge kutoka pande zote mbili watatoa rambirambi zao kufuatia kifo cha malkia. 

Jeneza la Malkia Elizabeth laanza safari ya mwisho Scotland

Baada ya hapo Mfalme Charles III Pamoja na mke wake Camilla watasafiri kwa ndege hadi Edinburgh kujiunga na ndugu zake kwenye msafara wa kusafirisha mwili wa malkia hadi kanisa la Mtakatifu Giles.

Maelfu kwa maelfu ya waombolezaji wamejitokeza barabarani kutoa heshima zao za mwisho. Mwili wa Malkia Elizabeth unatarajiwa kusalia kanisani humo wakati waombolezaji wakiruhusiwa kutoa heshima zao za mwisho. Mfalme Charles III atakuwa sehemu ya watakaokesha, kabla ya mwili kusafirisha kesho Jumanne kwa ndege hadi London.

Watu wajitokeza kutoa heshima zao za mwisho wakati mwili wa Malkia Elizabeth II ukisafirishwa kutoka Kasri la Balmoral kupelekwa Edinburgh. Septemba 11, 2022.
Watu wajitokeza kutoa heshima zao za mwisho wakati mwili wa Malkia Elizabeth II ukisafirishwa kutoka Kasri la Balmoral kupelekwa Edinburgh. Septemba 11, 2022.Picha: Jeff J Mitchell/Getty Images

Katika mataifa mengine, waombolezaji wamekuwa wakifika katika ofisi za ubalozi wa Uingereza kuwasilisha rambirambi zao mfano ni huyu Mirian Hernandez wa Ufilipino mkaazi wa Manila.

"Ninahisi kuwa huduma yake haikuwa kwa ajili ya nchi yake tu bali kwa kila mtu mwingine na inaathiri kila mtu duniani kote hivyo kuja hapa ni kuonyesha heshima na kumpa rambirambi zetu."

Mfahamu Malkia Elizabeth II

Tangu kifo cha Elizabeth aliyeaga akiwa na umri wa miaka 96 katika kasri lake la Balmoral, na aliyetawala kwa miaka 70, mfululizo wa mipango ya maombolezo imewekwa Uingereza.

Mnamo Jumapili, jeneza lililoubeba mwili wake, na kuwekewa shada la maua lilisafirishwa kwa gari kwa muda wa saa sita kutoka Balmoral hadi Edinburgh.

Mwili utakapowasili London siku ya Jumanne, kitakachofuata kuanzia Jumatano ni shughuli ya kitaifa ya mwili kutazamwa na watu hadi Septemba 19 atakapozikwa katika eneo la Westminister.
Mwili utakapowasili London siku ya Jumanne, kitakachofuata kuanzia Jumatano ni shughuli ya kitaifa ya mwili kutazamwa na watu hadi Septemba 19 atakapozikwa katika eneo la Westminister.Picha: James Manning/REUTERS

Inatarajiwa kuwa waombolezaji watajitokeza kwa wingi. Kupitia taarifa, serikali imesema wale wanaotaka kuutizama mwili kutoa heshima zao za mwisho watalazimika kusubiri kwa saa nyingi, labda hata usiku kucha kwenye foleni.

Hayo yakijiri, maelfu ya waombolezaji wanaj´zidi kumiminika katika makasri ya kifalme kote Uingereza kuweka mashada yam aua. Mjini London, foleni ndefu ya waombolezaji imeshuhudiwa katika bustani ya Green Park karibu na kasrli la Buckingham

Mara ya mwisho kwa tukio kama hilo la maombolezo kushuhudiwa Uingereza ni mwaka 1997, wakati mke wa kwanza wa Mfalme Charles, Princess Diana alipofariki mjini Paris kufuatia ajali ya gari barabarani.

(Vyanzo: Rtre, Fpe, Aptn)