Mfahamu Malkia Elizabeth II
9 Septemba 2022Uingereza inaomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II aliefariki akiwa na umri wa miaka 96, raia wake walimpenda malkia huyo kutokana na mengi aliyoyafanya katika utawala wake wa miaka 70, ametajwa kama kielelezo cha mfano halisi kwa taifa hilo liliopitia katika nyakati ngumu na nyepesi chini ya ufalme wake.
Malkia Elizabeth wa II aliongoza mataifa 16, malkia wa ufalme wa muungano Britania na Ireland ya Kaskazini pamoja na nchi za jumuiya madola lakini pia alikuwa mkuu wa kanisa la Anglikana.
Binti wa kifalme Elizabeth Alexandra Mary Windsor alizaliwa mnamo Aprili 21, 1926, huko London akiwa ni binti wa kwanza kwa mfalme George VI na Elizabeth Bowes-Lyon. Kwa wakati huo haikujulikana kama angelikuwa Malkia.
Soma pia:Viongozi wa Afrika waomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II
Hata hivyo alitokea kuwa kiongozi wa kifalme alie hai ambae alitawala kwa kipindi kirefu zaidi, malkia huyo alimwakilisha baba yake duniani kote kutokana na yeye kushindwa kuendelea na majukumu ya kiutawala sababu ya maradhi ya saratani ambapo hadi kufikia Februari 6 1952 alifariki na Malkia Elizabeth alitangazwa kuchukua hatamu akiwa nchini Kenya na kupewa taji rasmi Juni 2 1953 huko Westminster Abbey.
Mwanamfalme pekee alihudumu jeshi
Elizabeth alipata mafunzo ya ufundi magari na udereva ya magari makubwa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia na kwakipindi kirefu yeye likuwa mshiriki pekee wa familia ya kifalme aliyetumikia jeshi.
Harusi yake ilikuwa yakwanza katika familia ya kifalme barani Ulaya baada ya vita Novemba 20 1947, alipofunga pingu za maisha na Prince Philip Mountbatten, akiwa ni msaidizi katika familia za kifalme za Ugiriki na Denmerk ambae baadae alikuwa afisa katika jeshi la maji la kifalme na kupewa cheo cha juu cha Duke of Edinburgh muda mfupi kabla ya ndoa.
Alipovishwa taji mwaka wa 1953, Elizabeth aliapa kujitolea maisha yake kwa watu wa Britania, kiapo alichokipa uzito mkubwa.
Soma pia:Malkia Elizabeth II afariki dunia
Malkia alikuwa na wastani wa miadi rasmi 500 kwa mwaka kitu kilichomfanya kuwa kiongozi ambae asafiri zaidi katika historia.
Malkia Elizabeth II alikuwa ni mtu mwenye kulinda faragha zake na alikuwa na mapenzi makubwa kwa farasi na mbwa na pia alipenda mitindo yenye rangi za kuwaka.
Mawaziri wakuu 15 chini ya Malkia Elizabeth II
Wakati wa utawala wake, alisimamia mawaziri wakuu 15 wa Uingereza, kutoka Winston Churchill hadi Liz Truss ambaye alitegemea ushauri wake kwa kiwango kikubwa, ingawa alifanya juhudi kubwa kutobainisha maoni yake ya kisiasa kwa umma.Kila wiki, alipokea wanasiasa kwa mazungumzo yafaragha.
Soma pia:Ulimwengu unaomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II
Malikia Elizabeth II alisherehekea miaka 60 kama Malkia mnamo mwaka 2012 na pia aliwashangazawengi siku alipojitokeza akiwa na mcheza sinema ya James Bond Daniel Craig kwenye ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mwaka huo huko mjini London.