1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Mexico yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ecuador

6 Aprili 2024

Maafisa wa usalama wa Ecuador wamevamia ubalozi wa Mexico ulioko mjini Quito na kumkamata Makamu wa Rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas na kupelekea Mexico kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ecuador.

https://p.dw.com/p/4eUgg
Polisi wa Ecuador wakivamia Ubalozi wa Mexico mjini Quito
Maafisa wa usalama wa Ecuador walkivamia Ubalozi wa Mexico ulioko mjini Quito.Picha: IMAGO/Agencia Prensa-Independiente

Glas anayetafutwa kwa madai ya ufisadi amejificha kwa miezi kadhaa kwenye ubalozi wa Mexico, ulioko katika mji mkuu wa Ecuador, na mapema jana Ijumaa ubalozi wa Mexico ulitangaza kumpa hifadhi Glas, hatua iliyoichukuiza Ecuador.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Alicia Barcena amesema jana usiku kwamba taifa lake linavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ecuador mara moja na watawasilisha kesi hii mbele ya  Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ.

Barcena ameishutumu Mexico kwa kufanya ukiukwaji mkubwa wa Mkataba wa Vienna unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia kwa kuingia kwa nguvu kwenye ubalozi wake ili kumkamata Glas.