1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi ni mchezaji rasmi wa PSG sasa

11 Agosti 2021

Lionel Messi Jumatano alisema anafurahia kujiunga na klabu ya Ufaransa Paris Saint Germain PSG na kwamba yuko tayari kuisaidia timu hiyo kunyakua taji lake la kwanza la Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya, Champions League.

https://p.dw.com/p/3yqEA
Lionel Messi Press Conference after signing for Paris St Germain
Picha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

"Ndio sababu niko hapa," alisema Messi katika kikao na waandishi wa habari. "Wako tayari kupambana na kuwania kila kitu. Ndoto yangu ni kushinda taji lengine la Champions League na nafikiri hapa ndipo mahali sahihi kuwepo."

Messi ambaye ni raia wa Argentina lakini amesema hajui ni lini atakapocheza mechi yake ya kwanza kwani hajacheza tangu ashiriki fainali ya kombe la Copa America ambapo timu yake ya taifa iliibwaga Brazil.

Paris Lionel Messi trifft ein
Messi alipotua mjini ParisPicha: SARAH MEYSSONNIER/REUTERS

Messi ametia saini mkataba wa miaka miwili na miamba hao wa Ufaransa kukiwa na kipengee cha kuuongeza mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi.

Nyota huyo ambaye ameweka rekodi kwa kushinda tuzo ya mchezaji kandanda bora duniani mara sita, anajiunga na PSG kutoka Barcelona ambako aliichezea klabu hiyo ya Uhispania kwa kipindi cha miaka 21.