Meloni: Mashambulizi dhidi ya vikosi vya UNIFIL hayakubaliki
19 Oktoba 2024Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameshutumu mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL akisema hayakukubaliki. Kiongozi huyo wa Italia ameyasema hayo wakati wa ziara ya nchini Lebanon.
Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati, Meloni alisema kuwa jukumu la UNIFIL katika kanda hiyo bado ni muhimu. Hayo yanajiri baada ya kikosi cha UNIFIL kudai kuwa kifaru cha Israel kilishambulia mojawapo ya kituo chake na kusababisha uharibifu wa vifaa.
Wakati huo huo jeshi la Israel IDF limesema kuwa litapeleka kikosi cha ziada cha askari wa akiba kwenye mpaka wake na Lebanon wakati kikipambana na Hezbollah. Kundi hilo nalo limenukuliwa hapo jana likisema linaingia katika awamu mpya katika vita vyake dhidi ya Israel.