Meli kutoka Tanzania kuelekea Kongo yazama
8 Aprili 2024Hayo yakiarifiwa, watu 25 wameuwawa mashariki mwa Kongo kutokana na shambulio la waasi wa CODECO.
Meli hiyo ilikua na watu 26 wakiwemo raia 4 wa Tanzania, Mkenya mmoja, Wachina 4 na Wakongomani 17 kulingana na taarifa ya idara ya usafiri katika bandari ya kalemie.
Watu 15 wameokolewa huku maafisa wa uokoaji wakiendelea kutafuta wengine.
Upepo mkali ndio umesababisha ajali
Afisa tawala wa tarafa ya Kalemie John Mutombo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Abdul Ally Kayanda raia wa Tanzania ambaye ndugu yake amenusurika katika ajali hiyo ameiomba idara ya usafirishaji nchini Tanzania kudhibiti swala la upakiaji mizigo katika bandari ya Kigoma.
Idara ya uchukuzi katika bandari ya Kalemie kupitia kamishna wake Jean Kyato imesema kuwa chanzo cha ajali ni upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa.
Licha ya picha za mwisho za meli hiyo kuonesha imepakia mzigo mkubwa, afisa huyo amedai meli haikuwa imepakia zaidi ya uwezo wake.
Mili 25 imepatikana Ituri
Ajali hiyo imetokea sambamba na mauwaji ya watu 25 walio shambuliwa na waasi wa CODECO huko jimboni Ituri mashariki mwa Kongo ambapo mashirika ya kiraia pamoja na Umoja wa Mataifa wamethibitisha kutokea kwa shambulio hilo.
Taarifa kutoka huko zinasema miili 10 ilipatikana Jumamosi na 15 Jumapili katika kijiji cha Galayi, kilomita 70 kaskazini magharibi mwa mji wa Bunia,
Ikumbukwe kuwa hali ya kibinaadamu huko ituri imezorota tangu mwanzo wa mwaka huu kutokana na mashambulizi ya waasi wa CODECO, Ofisi ya pamoja ya haki za kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa (UNJHRC) ilisema.