Meli iliyobeba tani 30,000 za mafuta yawasili Lebanon
28 Agosti 2024Meli hiyo iliyobeba tani 30,000 za mafuta imewasili kwenye pwani ya kituo cha mafuta cha Tripoli, kaskazini mwa Lebanon.
Meli hiyo imeelekezwa na kutia nanga karibu na matangi ya kuhifadhi mafuta, ikitoa zawadi kutoka kwa serikali ya Algeria kuisaidia Lebanon kuendesha mitambo yake ya umeme.
Soma pia: Lebanon inaadhimisha miaka 4 tangu mlipuko wa bandari huku hofu ya vita ikitanda
Waziri huyo wa nishati wa Lebanon ameonyesha matumaini kuwa mitambo mikuu ya umeme ya nchi hiyo itaanza kufanya kazi ifikapo kesho Alhamisi, na kwamba ugavi wa umeme unatarajiwa kuongezeka hadi saa nne hadi sita kwa siku.
Mtambo wa mwisho wa umeme uliokuwa unafanya kazi katika nchi hiyo iliyokumbwa na mgogoro, ulifungwa katikati ya mwezi Agosti kutokana na ukosefu wa mafuta.