Lebanon inaadhimisha miaka 4 tangu mripuko wa bandari
4 Agosti 2024Matangazo
Maadhimisho hayo yanafanyika huku kukiwa na hofu ya kuanza kwa vita kamili kati ya Israel na kundi la Hezbollah.
Katika maadhimisho hayo maandamano kadhaa yatafanyika kwenye eneo la bandari majira ya mchana kwa madhumuni ya kudai haki na kuwakumbuka waathiriwa wa mripuko. Mamlaka za Lebanon zilieleza kuwa mripuko katika bandari ya Beirut ulisababishwa na moto uliotokea katika ghala moja lililokuwa likihifadhi mbolea ya ammonium nitrate kwa miaka mingi.
Uchunguzi kuhusu tukio hilo umekuwa ukisuasua huku ukigubikwa na mabishano ya kisheria na siasa. Hadi sasa hakuna yeyote aliyewajibishwa kwa tukio hilo la Agosti nne 2020, linalotajwa kuwa mripuko mkubwa zaidi usiohusisha nyuklia uliowajeruhi zaidi ya watu 6,500.