1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mchungaji Mackenzie ashtakiwa kwa mauaji Kenya

13 Agosti 2024

Kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili mchungaji Paul Mackenzie imeanza kusikilizwa mjini Mombasa, Kenya. Mackenzie anadaiwa kuwaamrisha wafuasi wafunge hadi kufa ili wakutane na Yesu.

https://p.dw.com/p/4jOgC
Kenya| Polisi ikimsindikiza Ezekiel Ombok Odero katika makao ya polisi mjini Mombasa
Mackenzie anashtakiwa pamoja na washukiwa wengine 93.Picha: Stringer/REUTERS

Kiongozi wa kidini aliewahimiza waumini wake kufunga hadi kufa nchini Kenya ameshtakiwa kwa mauaji ya bila kukusudia jana Jumatatu, kutokana na vifo vya watu zaidi ya 400 katika mmoja ya mikasa mibaya zaidi ya kidini duniani.

Waendesha mashtaka na maafisa wa mahakama wamesema Paul Mackenzie, aliejipa cheo cha uchungaji, alifikishwa mahakani mjini Mombasa pamoja na washukiwa wengine 93.

Mchungaji Paul Mackenzie mhakamani Mombasa.
Mchungaji Paul Mackenzie mhakamani Mombasa.Picha: Halima Gongo/DW

Soma pia: Mchungaji Mackenzie ashtakiwa kwa mauaji ya bila kukusudia Kenya

Mackenzie anadaiwa kuwachochea wafuasi wake kujinyima chakula hadi kufa ili waweze kukutana na Yesu, katika kisa kilichozusha taharuki nchini Kenya na duniani kote.

Alikamatwa mwezi Aprili mwaka jana, baada ya maiti kadhaa kugunduliwa katika eneo la mbali la msitu wa Shakahola, ulioko katika mji wa bahari ya Hindi wa Malindi.