1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema yataka tume yakuchunguza visa vya utekaji Tanzania

22 Agosti 2024

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume maalumu ya kimahakama kuchunguza matukio ya utekaji na utesaji raia yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jnTz
Tanzania I Siasa | Chadema | Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema Freeman Mbowe.Picha: Michael Jameson/AFP/Getty Images

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye amekutana na waandishi wa habari kufichua kadhia hiyo amesema kwa ujumla hali ni ya wasiwasi kufuatia kuzidi kuongezeka kwa matukio ya raia kutekwa na kupelekwa mafichoni.

Mbali ya kulinyoshea kidole jeshi la polisi, kiongozi huyo ametoa mwito kwa Rais Samia kunyosha mkono wake ili kuwaletea matumaini wale waliofikwa na mkasa hiyo ikiwamo ndugu na jamaa zao.

"Tunamtaka rais haraka atuundie taifa hili ili kurudisha amani na mshikamano na utulivu kwenye taifa, aunde tume ya kimahakama ichunguze haya yanayozungumza," alisema mwenyekiti huyo.

Aidha aliongeza kwamba kuundwa kwa tume hiyo mbali na mambo mengine itakuwa na jukumu la kuchunguza na kuwarejeshea watu uhuru wao katika njia ambazo ni za haki.

Soma pia:Chadema yaikosoa serikali baada ya kuteswa kwa viongozi wake

Hatua ya chama hicho kujitokeza hadharani kuzungumzia suala hilo inakuka suku chache baada ya chama cha wanasheria cha Tanganyika Law Society kurodhesha majina ya zaidi ya raia 80 ambao wanadaiwa kutekwa na kuteswa katika maeneo mbalimbali huku jiji la Dar es salaam likiongoza kwa idadi ya matukiuo hayo.

Ama baadhi ya wale wanaotajwa kufikwa na madhila ya kutesa na wengine jamaa zao kufikwa na kadhia hiyo walijitokeza katika mkutano wa Chadema wakionyesha hisia za kuomba msaada.

Mgoggoro wa Ngorongoro

Kuhusu yale yanayoendelea katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambako serikali imetangaza kufuta vijiji pamoja na kusitisha huduma za kijamii kwa jamii wa maasai, Chadema imesema hatua hiyo haiwezi kuwa mwarobaini wa kumaliza mvutano unaoendelea.

"Wamasai wa Ngorongoro wahamishwe kwa ridhaa yao kutokana na na ushawishi watakaopewa" Alisema Mbowe kwenye mazungumzo yake na waandishi wa habari.

Baadhi ya wamasai Tanzania waandamana kupinga kuondoshwa eneo la hifadhi

Soma pia:TLS yakosoa kile kinachoendelea dhidi ya Wamaasai walioko Ngorongoro

Serikali imekuwa ikiendesha operesheni maalumu inayoitwa operesheni ya hiari ya kuwahamisha jamii ya wamasai katika eneo hilo na kuwapeleka eneo la Msomera mkoani Tanga katika kile inachosema kujaribu kunusuru hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kutumbukia katika uharibofu wa kimazingira.