1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Haftar afanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin mjini Moscow

29 Septemba 2023

Ikulu ya Kremlin imesema mbabe wa kivita Khalifa Haftar, ambaye vikosi vyake vinatawala upande wa mashariki mwa Libya, amefanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4WwG7
Mbabe wa kivita nchini Libya Khalifa Haftar
Mbabe wa kivita nchini Libya Khalifa HaftarPicha: Abdullah Doma/AFP/Getty Images

Vikosi vyake pia vimethibitisha mkutano huo kwa kuandika kwenye ukurusa wao rasmi wa Facebook kuwa, Haftar amefanya mazungumzo na Rais Putin na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu bila ya kutoa maelezo zaidi.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ameeleza kuwa, Haftar na Putin wamejadili juu ya hali ya mambo nchini Libya na ukanda huo kwa ujumla.

Kulingana na vyombo vya habari vya Libya, huo ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya wawili hao tangu mwaka 2019.

Haftar anayeongoza utawala hasimu kwa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli, kwa muda mrefu amedumisha uhusiano na Moscow na anategemea sana msaada wa kijeshi kutoka kundi la mamluki la Urusi la Wagner.