Haftar atoa kitishi kipya kuhusiana na mapato ya mafuta
4 Julai 2023Matangazo
Haftar amesema inabidi paundwe kamati ya kuweka utaratibu wa kusimamia masuala ya kifedha kwa lengo la kuwa na usimamizi wa haki wa fedha za umma. Ikiwa hatua hiyo haitofanyika ataliamrisha jeshi lake kuchukua hatua.
Akizungumza katika mji wa Rajma karibu na Benghazi,Haftar ametangaza mwisho wa mwezi Agosti kuwa muda wa mwisho wa kamati hiyo kukamilisha kazi yake.
Mwishoni mwa mwezi uliopita kiongozi wa utawala wa upande wa Mashariki, Oussama Hamad alitishia kuzuia usafirishaji wa mafuta na gesi kutokea eneo hilo la Mashariki, akidai kwamba serikali ya mjini Tripoli inafuja mapato yanayotokana na nishati hiyo.