1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya usitishaji vita Gaza kuanza tena Cairo kesho

2 Machi 2024

Mazungumzo ya usitishaji vita Gaza yanatarajiwa kuanza tena mjini Cairo kesho Jumapili, vimesema vyanzo viwili vya usalama katika ishara ya kuendelea kwa juhudi za upatanishi.

https://p.dw.com/p/4d6e5
Ukanda wa Gaza | Wapalestika wakiwa katika sala ya pamoja
Baadhi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza wakiwa katika sala ya pamoja.Picha: Mohammed Salem/REUTERS

 Hakukuwa na kauli kutoka Israel au kundi la Hamas, ambao wamekuwa wakijadiliana kupitia wapatanishi wakiwemo Misri na Qatar.

Vyanzo hivyo vimesema tukio la Alhamisi ambapo zaidi ya watu 100 waliuawa na wanajeshi wa Israel, halijapunguza kasi ya mazungumzo, bali limewasukuma wapatanishi kulinda maendeleo yaliofikiwa.

Soma pia:Israel yazidisha mashambulizi Gaza baada ya turufu ya Marekani UM

Shinikizo la kimataifa limeongezeka kusisitisha vita hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 30,000, huku Umoja wa Mataifa ukionya kwamba robo ya wakaazi wa Gaza wako kwenye hatari kubwa ya kufa kwa njaa.