Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuiwekea viongozi Niger
31 Agosti 2023Katika mkutano unaojadili juu ya vikwazo vinavyowalenga watawala wa kijeshi nchini Niger waliotwaa madaraka kwa nguvu mwezi mmoja uliopita.
Wengi wa mawaziri hao wamesema kwamba bara la Afrika linapaswa kushughulikia changamoto zake.
Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Antonio Tajani amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kutetea demokrasia kwa njia za kidiplomasia na sio kupitia matumizi ya silaha.
Soma pia:Umoja wa Ulaya kuijadili Niger katika mkutano maalum
Tajani ametahadharisha dhidi ya uingiliaji wa kijeshi nchini Niger akisema kwamba ni hatua itakayosababisha hatari ya kuwaacha watu wengi zaidi bila makaazi katika eneo la Sahel.
Mawaziri hao wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana Toledo Uhispania wamesema ni muhimu kuiunga mkono jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.
Mawaziri hao pia wanajadili pamoja na waziri mwenzao wa Ukraine, kuhusu kampeini ya juhudi za kidiplomasia ya Ukraine kumaliza uvamizi wa Urusi nchini humo.