1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuijadili Niger katika mkutano maalum

31 Agosti 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Toledo Uhispania, ambapo mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja huo Josep Borrell, atapendekeza juu ya vikwazo dhidi ya waliohusika na mapinduzi Niger.

https://p.dw.com/p/4VnWx
Belgien EU-CELAC Josep Borrell im Gebäude des Europäischen Rates in Brüssel
Picha: Francois Walschaerts/AP Photo/picture alliance

Borrell amesema  uamuzi juu ya vikwazo vitakavyopitishwa na Umoja huo  unalenga kwenda sambamba na hatua zozote zitakazochukuliwa  na nchi za kikanda za jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS. 

Soma pia:EU yazingatia majibu yake kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger

Mkuu huyo wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya akizungumza mbele ya waandishi habari baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi jana Jumatano huko Toledo alisema watafuata mwelekeo wa kujaribu kutekeleza vikwazo kama ilivyoamuliwa  na ECOWAS.

Kadhalika amesema Umoja huo unaweza kufikiria kutoa msaada wa fedha kwa ECOWAS iwapo jumuiya hiyo itataka kuingia kijeshi Niger na ikiwa itaomba msaada huo.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW